About Us   |   Contact Us   |  
Submission  

Ubainishaji wa Maswali ya Balagha kwa Kuzingatia Viashiria vya Kimofolojia katika Mazungumzo ya Kiswahili

DOI : https://doi.org/10.36349/easjehl.2025.v08i05.001
PDF
HTML
XML

Abstract: Makala hii inahusu ubainishaji wa maswali ya balagha kwa kuzingatia viashiria vya kimofolojia katika mazungumzo ya Kiswahili. Maswali ya balagha ni maswali yasiyohitaji majibu yenye lengo la kufikisha ujumbe kwa wahusika. Maswali haya hutumika kama mbadala wa kauli mbalimbali. Ili kupata kile kilichokusudiwa, maswali haya hayana budi kubainishwa. Suala la ubainishaji wa maswali ya balagha hutofautiana kulingana na lugha. Kwa kuwa suala la ubainishaji wa maswali ya balagha katika Kiswahili haliko bayana, makala hii inalenga kutoa maarifa hayo kwa kuonesha viashiria vya kimofolojia vinavyotumika kubainisha maswali ya balagha katika mazungumzo ya Kiswahili. Data za Makala hii zilipatikana kutoka katika mazungumzo ya kwenye vibanda vya mpira, mamantilie na vijiwe vya bodaboda kutoka mikoa ya Dar es Salaam na Mbeya. Mbinu ya ushuhudiaji wa kushiriki ilitumika kukusanya data. Aidha, uchambuzi wa data umefanywa kwa kutumia mkabala wa maelezo. Nadharia ya Tendo-uneni ya Searle (1979) imetumika katika ukusanyaji na uchambuzi wa data za Makala hii. Matokeo yanaonesha kuwa katika mazungumzo ya Kiswahili, maswali ya balagha huweza kuashiriwa na viashiria vya kimofolojia. Kuna viashiria kama vialami pragmatiki, viunganishi na vitenzi ambavyo huukilia fasiri ya kibalagha. Makala hii inabainisha kuwa pamoja na kwamba kuna viashiria vya kimofolojia, bado muktadha wa mazungumzo ndio unaovifanya vipate nguvu ya kubainisha maswali ya balagha. Makala hii inapendekeza tafiti nyingine zifanyike katika miktadha tofautitofauti ili kuendelea kuweka bayana suala la ubainishaji wa maswali ya balagha katika Kiswahili kwa ajili ya kujenga maarifa ya kisemantiki na kipragmatiki.

TOP EDITORS

OPEN ACCESS JOURNALS

Dr. Afroza Begum

Lecturer, Dept. of Pharmacology and Therapeutics, Shaheed Monsur Ali Medical College & Hospital, Uttara, Dhaka-1230, Bangladesh

BEST AUTHOR

Of The Month

TRACK YOUR ARTICLE

Enter the Manuscript Reference Number (MRN)
Get Details

Contact us


EAS Publisher (East African Scholars Publisher)
Nairobi, Kenya


Phone : +91-9365665504
Whatsapp : +91-8724002629
Email : easpublisher@gmail.com

About Us


EAS Publisher (East African Scholars Publisher) is an international scholar’s publisher for open access scientific journals in both print and online publishing from Kenya. Its aim is to provide scholars ... Read More Here

*This work is licensed under a Creative Commons Attribution-NonCommercial 4.0 International License.

© 2020, All Rights Reserved | SASPR Edu International Pvt. Ltd.

Developed by JM