About Us   |   Contact Us   |  
Submission  

Dosari za Kimofosintaksia Zinazofanywa na Wajifunzaji wa Kiswahili katika Shule za Sekondari Nchini Uganda

DOI : https://doi.org/10.36349/easjehl.2025.v08i05.002
PDF
HTML
XML

Wajifunzaji wa lugha ya pili hufanya dosari mbalimbali za kiisimu katika ujifunzaji wao. Tafiti mbalimbali kuhusu suala hili zinaonesha kuwa dosari katika ujifunzaji wa lugha ya pili au lugha ya kigeni hutokea kama athari za lugha za kwanza za wajifunzaji. Mwandishi wa makala haya alikisia kuwa dosari zinazofanywa na wajifunzaji wa Kiswahili hazitokani na athari za lugha za kwanza pekee, bali kuna masuala mengine yanayowasababishia wajifunzaji kufanya dosari katika ujifunzaji wa Kiswahili kama lugha ya pili. Hali hii ndiyo iliyochochea raghba ya kufanyika kwa utafiti huu unaohusu dosari za kimofosintaksia zinazofanywa na wajifunzaji wa Kiswahili katika shule za sekondari nchini Uganda. Makala haya ni sehemu ya tasnifu ya uzamivu ya mwandishi wa makala. Data ya utafiti uliozaa makakala haya ilikusanywa kwa kutumia uchambuzi matini pamoja na ushuhudiaji. Uchanganuzi wa data uliongozwa na Nadharia ya Usasanyuzi Dosari iliyoasisiwa na Corder (1967). Matokeo ya uchambuzi wa data yamebainisha kuwa wajifunzaji wa Kiswahili katika shule za sekondari nchini Uganda hufanya dosari mbalimbali za kimofosintaksia. Dosari hizo ni pamoja na matumizi yasiyo sahihi ya vipatanishi vya kisarufi, matumizi yasiyo sahihi ya viambishi, vielezi, virejeshi, vivumishi, kuchanganya njeo, utohozi usiofaa pamoja na kutokukanusha kwa usahihi.

TOP EDITORS

OPEN ACCESS JOURNALS

Dr. Afroza Begum

Lecturer, Dept. of Pharmacology and Therapeutics, Shaheed Monsur Ali Medical College & Hospital, Uttara, Dhaka-1230, Bangladesh

BEST AUTHOR

Of The Month

TRACK YOUR ARTICLE

Enter the Manuscript Reference Number (MRN)
Get Details

Contact us


EAS Publisher (East African Scholars Publisher)
Nairobi, Kenya


Phone : +91-9365665504
Whatsapp : +91-8724002629
Email : easpublisher@gmail.com

About Us


EAS Publisher (East African Scholars Publisher) is an international scholar’s publisher for open access scientific journals in both print and online publishing from Kenya. Its aim is to provide scholars ... Read More Here

*This work is licensed under a Creative Commons Attribution-NonCommercial 4.0 International License.

© 2020, All Rights Reserved | SASPR Edu International Pvt. Ltd.

Developed by JM