About Us   |   Contact Us   |  
Submission  

Mawasiliano Bora au Migogoro: Athari Zinazotokana na Matumizi ya Upole Katika Longalonga za Wanabodaboda na Abiria

DOI : https://doi.org/10.36349/easjehl.2025.v08i07.002
PDF
HTML
XML

Upole ni mojawapo ya mitindo ambayo watu hutumia ili kufikia azma zao za mawasiliano. Utafiti huu ulilenga kuchunguza athari zinazotokea kwa kutumia au kutotumia mikakati ya upole katika mawasiliano. Ni utafiti wa kithamano uliofanyika katika kaunti ndogo ya Mbooni, kaunti ya Makueni, nchini Kenya. Nadharia ya upole ilitumika kama kielelezo. Ili kupata watafitiwa walio na sifa za kudhihirisha uwezo wa kujibu maswali ya utafiti, usampulishaji wa kimakusudi ulitumika. Mahojiano na uchunzaji ndizo mbinu zilizotumika kukusanya data. Data iliyopatikana ilihawilishwa kutoka kwa lugha ya Kikamba hadi ya Kiswahili kwa kutumia tafsiri huru. Data hii iliweza kusimbwa kwa ajili ya uchanganuzi. Uchanganuzi wa data ulihusisha uhakiki wa kina wa majibu ya wahojiwa na baadhi ya kauli za wahudumu wa bodaboda na abiria. Uchanganuzi huu ulinuia kuonyesha athari za kutumia au kutotumia mikakati ya upole kwa mawasiliano ya wahudumu wa bodaboda na abiria. Matokeo ya utafiti huu yalionyesha kuwa matumizi ya mikakati ya upole huwa na athari chanya kwa mawasiliano kama vile; kudumisha heshima, kuleta athari ya raghba, kuokoa muda, kufanikisha mawasiliano, kupoza hisia za hasira na kujenga mahusiano thabiti kati ya wahudumu wa bodaboda na abiria. Kwa upande mwingine ukiukaji wa matumizi ya mikakati ya upole ulidhihirisha athari hasi kwa mawasiliano kama vile kutishia uso wa msikilizaji na kukatika kwa mawasiliano. Utafiti huu una mchango muhimu katika nyanja za mawasiliano hasa kwa kuimarisha maingiliano ya wahusika katika muktadha wa uchukuzi na mawasiliano ya jamii kwa jumla.

TOP EDITORS

OPEN ACCESS JOURNALS

Dr. Afroza Begum

Lecturer, Dept. of Pharmacology and Therapeutics, Shaheed Monsur Ali Medical College & Hospital, Uttara, Dhaka-1230, Bangladesh

BEST AUTHOR

Of The Month

TRACK YOUR ARTICLE

Enter the Manuscript Reference Number (MRN)
Get Details

Contact us


EAS Publisher (East African Scholars Publisher)
Nairobi, Kenya


Phone : +91-9365665504
Whatsapp : +91-8724002629
Email : easpublisher@gmail.com

About Us


EAS Publisher (East African Scholars Publisher) is an international scholar’s publisher for open access scientific journals in both print and online publishing from Kenya. Its aim is to provide scholars ... Read More Here

*This work is licensed under a Creative Commons Attribution-NonCommercial 4.0 International License.

© 2020, All Rights Reserved | SASPR Edu International Pvt. Ltd.

Developed by JM