About Us   |   Contact Us   |  
Submission  

Balagha kama Ulimbo uliotumiwa kunasia Uungwaji mkono katika Makongamano ya Wagombea Wawili wa Urais nchini Kenya Mwaka wa 2022

DOI : https://doi.org/10.36349/easjehl.2025.v08i08.003
PDF
HTML
XML

Katika mazingira mbalimbali ya kijamii na ya kisiasa, balagha ni mkakati wa mawasiliano unaotumika kwa lengo la kushawishi. Utafiti huu ulilenga kuchanganua kwa kina sababu zilizosababisha matumizi ya balagha katika hotuba za wagombea wawili wa urais, wakati wa makongamano yao ya kitaifa ya wajumbe nchini Kenya, mwaka wa 2022. Wagombea hao walikuwa William Samoei Ruto na Raila Odinga. Nadharia ya Balagha ya Aristotle iliongoza utafiti huu. Ilisaidia mtafiti katika kutambua sababu za matumizi ya balagha, kama ilivyothibitika katika hotuba nne zilizowasilishwa. Data ya utafiti huu ilikusanywa kutoka kwa rekodi rasmi za hotuba hizo kutoka kwa mtandao wa YouTube. Mbinu ya usampulishaji wa kimakusudi ilitumika kuchagua hotuba za wagombea hawa kwa kuzingatia nafasi zao za kisiasa na ushawishi waliokuwa nao katika uchaguzi mkuu wa 2022. Hii ni kutokana na uzoefu wao wa muda mrefu katika siasa na nafasi yao ya kipekee katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2022. Data ilichanganuliwa kwa njia ya kimaelezo. Utafiti uligundua kuwa balagha ilitumika hasa kwa nia ya kujenga imani, kugusa hisia, kuumua mihemko miongoni mwa wasikilizaji, kudhihirisha mantiki, kujenga imani mbele ya hadhira, kudhihirisha tajriba katika utekelezaji wa majukumu, kujinasibisha na hadhira, kuelekeza mtazamo wa hadhira na kushinda uchaguzi. Utafiti uligundua kuwa balagha ilitumika hasa kujenga imani ya wagombea, kugusa hisia na kueleza sera zao. Utafiti ulihitimisha kuwa balagha ina jukumu muhimu katika mawasiliano ya kisiasa na ushawishi wa hadhira lengwa.

TOP EDITORS

OPEN ACCESS JOURNALS

Dr. Afroza Begum

Lecturer, Dept. of Pharmacology and Therapeutics, Shaheed Monsur Ali Medical College & Hospital, Uttara, Dhaka-1230, Bangladesh

BEST AUTHOR

Of The Month

TRACK YOUR ARTICLE

Enter the Manuscript Reference Number (MRN)
Get Details

Contact us


EAS Publisher (East African Scholars Publisher)
Nairobi, Kenya


Phone : +91-9365665504
Whatsapp : +91-8724002629
Email : easpublisher@gmail.com

About Us


EAS Publisher (East African Scholars Publisher) is an international scholar’s publisher for open access scientific journals in both print and online publishing from Kenya. Its aim is to provide scholars ... Read More Here

*This work is licensed under a Creative Commons Attribution-NonCommercial 4.0 International License.

© 2020, All Rights Reserved | SASPR Edu International Pvt. Ltd.

Developed by JM