About Us   |   Contact Us   |  
Submission  

Machozi Ya Kimya: Athari Za Unyanyasikaji Wa Wanaume Katika Diwani Za Tumbo Lisiloshiba Na Maskini Milionea Na Hadithi Nyingine

DOI : https://doi.org/10.36349/easjehl.2025.v08i09.004
PDF
HTML
XML

Fasihi kama kioo cha jamii hutumia lugha kwa ufanifu mkubwa kutuchorea taswira kamili ya yale yanayotendeka katika jamii. Utafiti huu uliangazia unyanyasikaji wa wanaume katika hadithi fupi teule za Kiswahili. Ulichunguza suala la ukiukaji wa haki za wanaume kama ilivyosawiriwa katika hadithi fupi teule katika Diwani za Tumbo Lisiloshiba na Hadithi Nyingine na Maskini Milionea na Hadithi Nyingine. Lengo kuu la makala hii ni kuchunguza Machozi ya Kimya: athari za unyanyasikaji wa wanaume katika diwani teule. Ili kuafikia lengo hili, nadharia ya Mtagusano wa Vitambulisho ilitumiwa. Ni mojawapo ya nadharia za kijinsia. Utafiti huu ulikuwa wa kimaktaba. Data ya utafiti ilikusanywa kwa kusoma hadithi teule kutoka diwani za Kiswahili zilizoteuliwa vitabu, majarida na makala mengine kutoka mitandaoni. Uteuzi wa sampuli ulikuwa wa kimaksudi. Data iliyokusanywa ilichanganuliwa kimaelezo kwa kutumia mbinu ya uchanganuzi matini ikiongozwa na madhumuni ya utafiti. Matokeo ya utafiti yaliwasilishwa kwa njia ya kimaelezo. Matokeo ya makala yalionyesha kuwa mwanamume huathirika kwa namna nyingi kama vile: majuto, kukata tamaa, ukosefu wa amani, majeraha ya mwili, upweke, kuvunjika kwa ndoa na msongo wa mawazo. Vipengele vya utambulisho vinavyoshirikiana na kusababisha kunyanyasika na kuathirirka kwa wanaume ni: uchumi, jinsia, tabaka, matarajio ya kijamii. Kipengele kinachosababisha kunyanyasika na kuathirika kwa wanaume zaidi ni kipengele cha uchumi. Uchunguzi huu utawafaa wasomi, wanajamii, na waandishi kwani watapata uelewa zaidi wa aina za unyanyasikaji unaotendewa wanaume na kutafuta mbinu za kuwaokoa kutoka kwa udhalimu huu. Vile vile utakuwa na mchango katika taaluma ya fasihi ya Kiswahili.

TOP EDITORS

OPEN ACCESS JOURNALS

Dr. Afroza Begum

Lecturer, Dept. of Pharmacology and Therapeutics, Shaheed Monsur Ali Medical College & Hospital, Uttara, Dhaka-1230, Bangladesh

BEST AUTHOR

Of The Month

TRACK YOUR ARTICLE

Enter the Manuscript Reference Number (MRN)
Get Details

Contact us


EAS Publisher (East African Scholars Publisher)
Nairobi, Kenya


Phone : +91-9365665504
Whatsapp : +91-8724002629
Email : easpublisher@gmail.com

About Us


EAS Publisher (East African Scholars Publisher) is an international scholar’s publisher for open access scientific journals in both print and online publishing from Kenya. Its aim is to provide scholars ... Read More Here

*This work is licensed under a Creative Commons Attribution-NonCommercial 4.0 International License.

© 2020, All Rights Reserved | SASPR Edu International Pvt. Ltd.

Developed by JM