About Us   |   Contact Us   |  
Submission  

Mchango wa Upeaji wa Utambulisho Katika Diskosi za Wabunge Wanawake Kuhusiana na Mamlaka Katika Bunge la Taifa la Kenya

DOI : https://doi.org/10.36349/easjehl.2025.v08i09.006
PDF
HTML
XML

Diskosi za kisiasa za wanawake zina mchango muhimu katika kuthibiti mamlaka katika jamii ambayo imetawaliwa na wanaume. Kupitia uchunguzi wa lugha, utambulisho wa mwanasiasa na ushirika wake kwa vikundi maalumu unaweza kujitokeza kupitia upeaji wa kiutambulisho. Utafiti huu umechunguza mchango wa upeaji wa utambulisho katika diskosi za wabunge wanawake kuhusiana na mamlaka katika Bunge la Taifa la Kenya. Utafiti huu umeongozwa na nadharia ya Uchanganuzi wa Peo na mtazamo wa Uchanganuzi Hakiki-Makinifu wa Usemi. Nadharia hizi zilitumika kutathmini mchango wa upeaji wa utambulisho kwenye diskosi za wabunge wanawake wakati wa kuunda utambulisho kuhusiana na mamlaka. Chanzo cha data ya utafiti huu ilikuwa video ambazo zilikuwa zimehifadhiwa katika mtandao wa YouTube, kutoka kwa hotuba za wabunge wanawake 169, waliochaguliwa na wapiga kura katika bunge la 11, 12 na 13 la taifa la Kenya. Wasailiwa walikuwa wanawake 111 waliochaguliwa kuwakilisha kaunti pamoja na wanawake 58 waliochaguliwa kuwakilisha maeneobunge mbalimbali katika Bunge la Taifa. Mbinu ya utafiti iliyotumika kukusanywa data ilikuwa utazamaji na usikilizaji wa sauti ninga kutoka kwa mtandao ya YouTube. Utafiti huu umebaini kuwa. upeaji wa utambulisho huwa na dhima zifuatazo: dhima ya kudumisha mamlaka ya jinsia ya kike dhidi ya mabadiliko, kukarabati hali ante kwa njia ya kupanua wa mamlaka na kubadilisha mahusiano ya mamlaka yaliyopo baina ya jinsia.

TOP EDITORS

OPEN ACCESS JOURNALS

Dr. Afroza Begum

Lecturer, Dept. of Pharmacology and Therapeutics, Shaheed Monsur Ali Medical College & Hospital, Uttara, Dhaka-1230, Bangladesh

BEST AUTHOR

Of The Month

TRACK YOUR ARTICLE

Enter the Manuscript Reference Number (MRN)
Get Details

Contact us


EAS Publisher (East African Scholars Publisher)
Nairobi, Kenya


Phone : +91-9365665504
Whatsapp : +91-8724002629
Email : easpublisher@gmail.com

About Us


EAS Publisher (East African Scholars Publisher) is an international scholar’s publisher for open access scientific journals in both print and online publishing from Kenya. Its aim is to provide scholars ... Read More Here

*This work is licensed under a Creative Commons Attribution-NonCommercial 4.0 International License.

© 2020, All Rights Reserved | SASPR Edu International Pvt. Ltd.

Developed by JM