About Us   |   Contact Us   |  
Submission  

Mofu za Nafsi katika Muundo wa Kitenzi cha Lahaja ya Kimakunduchi

DOI : https://doi.org/10.36349/easjehl.2026.v09i04.009
PDF
HTML
XML

Mofu za nafsi ni vipashio vya msingi katika muundo wa vitenzi vya lugha za Kibantu. Dhima kuu ya mofu hizi ni kutoa upatanisho wa kisarufi kwa nomino au kiwakilishi mtenda au mtendwa katika tungo. Makala hii ilichunguza maumbo ya mofu za nafsi katika kitenzi cha lahaja ya Kimakunduchi. Uchunguzi huo umezingatia sifa za mofu hizo kimofofonolojia na kimofosintaksia. Katika viwango hivi mofu za nafsi zilichunguzwa katika mitindo na maumbo mbalimbali yaliyoathirika kifonolojia, ilhali hubeba dhima moja ya kimuundo na kiutendaji katika tungo husika. Pia mofu zilichunguzwa katika midhihiriko yake kimuonekano, kinafasi na kiutendakazi. Data za utafiti huu zilikisanywa kutoka shehia ya Nganani, Kibanguni na Kae-kuu kwa kutumia usimulizi na ushuhudiaji-shiriki. Utafiti huu ulitumia Nadharia ya Kanuni Finyizi iliyoasisiwa na Noam Chomsky (1995: 2000: 2001). Misingi mikuu ya nadharia hii ni umbo fonetiki na umbo mantiki ikimaanisha sauti na maana rejelewa ya sauti hizo zinazotokana na umilisi na utendaji wa wazawa. Katika kazi hii, mofu za nafsi hurejelewa kama vipatanishi vya kiima (Upk) au vipatanishi vya yambwa (Upy). Matokeo ya utafiti huu yanaonesha kuwa mofu za nafsi kama vipatanishi kiima na yambwa hudhihirika katika nafasi ya kiambishi awali katika kitenzi vikiwa katika hali ya dhahiri, mficho au jumuishi, kulingana na mazingira ya kifonolojia, kimuundo na umilisi wa wazungumzaji wazawa. Nafasi ya udhihirikaji wa mofu za nafsi ina athari muhimu za kimofosintaksia na kisemantiki.

TOP EDITORS

OPEN ACCESS JOURNALS

Professor Thomas Count Dracula, MD, PhD

Distinguished Professor of Haematology Head — Experimental, Historical & Sensory Haematology Vlad the Impaler University, Wolf’s Lane, Wooden Stakes Grove 666, Transylvania.

BEST AUTHOR

Of The Month

TRACK YOUR ARTICLE

Enter the Manuscript Reference Number (MRN)
Get Details

Contact us


EAS Publisher (East African Scholars Publisher)
Nairobi, Kenya


Phone : +91-9365665504
Whatsapp : +91-8724002629
Email : easpublisher@gmail.com

About Us


EAS Publisher (East African Scholars Publisher) is an international scholar’s publisher for open access scientific journals in both print and online publishing from Kenya. Its aim is to provide scholars ... Read More Here

*This work is licensed under a Creative Commons Attribution-NonCommercial 4.0 International License.

© 2020, All Rights Reserved | SASPR Edu International Pvt. Ltd.

Developed by JM