About Us   |   Contact Us   |  
Submission  

Athari za Ujinsia Unaodokezwa katika Majina ya Watu ya Jamiilugha za Kibantu Nchini Tanzania

DOI : https://doi.org/10.36349/easjehl.2026.v09i09.003
PDF
HTML
XML

Majina ya watu hayatumiki kama utambulisho wa watumiaji wake pekee, bali ni nyenzo inayotumiwa na wanajamii kuendeleza amali, tamaduni, historia, mamlaka, na mahusiano ya wanajamii. Makala hii imechunguza athari za ujinsia unaodokezwa katika majina ya watu ya jamiilugha za Kibantu nchini Tanzania kwa watumiaji wa majina husika. Data za utafiti huu zilikusanywa kutoka katika jamiilugha za Kiswahili, Kinyakyusa, Kisambaa, Kigogo, Kisukuma, na Kiha katika mikoa ya Dar es Salaam, Mbeya, Tanga, Dodoma, Mwanza, na Kigoma. Aidha, data hizo zilikusanywa kwa njia ya usaili na majadiliano katika makundi lengwa kutoka kwa watoataarifa 240 wa umri wa zaidi ya miaka 25. Kadhalika, data zilikusanywa na kuchanganuliwa kitaamuli kwa kutumia mbinu ya uchanganuzi wa maudhui na kuongozwa na Nadharia ya Ubabedume ya Bly (1970). Kwa ujumla, imebainika kuwa athari za ujinsia unaodokezwa katika majina ya watu kwa watumiaji wake ni kuwa ujinsia hujenga na kuimarisha tabia za wanajamii, huukilia mamlaka za watu katika familia na jamii, na husababisha matatizo ya kisaikolojia kwa wanajamii. Athari zingine za ujinsia ni kuwa huukilia mahusiano ya wanajamii kwa Mungu na wahenga, huukilia mafanikio ya wanajamii, hudhibiti mawanda ya upataji maarifa kwa wanajamii, na huchochea wanajamii kuchukia lugha na tamaduni zao. Hivyo basi, makala hii inatoa rai kuwa mamlaka za utoaji wa majina ya watu ziweke umuhimu mkubwa katika mchakato wa utoaji wa majina ya watoto kwani majina hayapo kwa ajili ya utambulisho pekee, bali ni nyenzo madhubuti ya kufinyanga na kuamua mwelekeo na hatma za maisha ya wanajamii na jamii kwa ujumla.

TOP EDITORS

OPEN ACCESS JOURNALS

Professor Thomas Count Dracula, MD, PhD

Distinguished Professor of Haematology Head — Experimental, Historical & Sensory Haematology Vlad the Impaler University, Wolf’s Lane, Wooden Stakes Grove 666, Transylvania.

BEST AUTHOR

Of The Month

TRACK YOUR ARTICLE

Enter the Manuscript Reference Number (MRN)
Get Details

Contact us


EAS Publisher (East African Scholars Publisher)
Nairobi, Kenya


Phone : +91-9365665504
Whatsapp : +91-8724002629
Email : easpublisher@gmail.com

About Us


EAS Publisher (East African Scholars Publisher) is an international scholar’s publisher for open access scientific journals in both print and online publishing from Kenya. Its aim is to provide scholars ... Read More Here

*This work is licensed under a Creative Commons Attribution-NonCommercial 4.0 International License.

© 2020, All Rights Reserved | SASPR Edu International Pvt. Ltd.

Developed by JM